Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mastaa wa Bongo wenye mikoko 2023

Tukiwa tupo katika kumaliza robo ya mwisho wa mwaka 2023 sasa leo nakutajia orodha ya mastaa wa Bongo waliotisha kwa kumiliki mikoko mikali na mipya ambao ni BillNass, S2Kizzy, Chino Kid, Platform, Gigy Money, Paula Kajala,Hamisa Mobetto, Wema sepetu, Zuchu, Nay Wamitego na DJ Ally B. Na 80% kati yao wamevuta ndinga aina ya Range Rover.

Aprili 12, mwaka huu usiku huo ilikuwa ni birthday party ya staa wa muziki, Billnass na miongoni mwa matukio ni pale mke wa staa huyo Nandy alipomzawadia mumewe Gari aina ya Range Rover mpya kabisa ya rangi ya Silver.

Baada ya Billnass kupewa zawadi hiyo naye staa wa muziki Zuchu akaweka kuwa atajizawadia na yeye Range, basi siku mbili baadae akashare nasi gari aina ya Range nyeusi hiyo akawa miongoni mwa walio na mkoko wa Range.

Ndani ya mwezi huo huo pia rapa Nay wa Mitego akaweka wazi kununua Range yake. Nayeye akaingia Team Range akiwakilisha wasanii wa Hip Hop.

Mrembo Paula Kajala ambye ni mpenzi wa staa wa muziki Marioo, Mwezi May anunua gari yake ya pili ambayo alidai kunua kwa pesa yake mwenyewe million 45 na gari hiyo ni Toyota Vanguard

Julai mwaka huu one of sex lady kutoka hapa 255 Hamisa Mobetto alikwea pipa hadi kuifuata zawadi yake ya aliyojinunulia ni gari mpya aina ya ‘Range Rover Velar’. Na DJ Ally B pia ASUMANII mwezi huo na yeye alivuta ndinga aina ya Range Rover.
Mwezi Julai haukupoa pia naye Gigy Money alinunua gari jipya aina ya Harrier lenye thamani ya Milioni 45 na Tanzania Sweetheart pia Wema Sepetu anunua gari la Milioni 100.

Pia uongozi wa Abbah Music ulimzawadia msanii wake Platform gari mpya aina ya ‘Crown New Model’.

Na wiki tano zilizopita Dansa wa Marioo ambaye pia ni msanii wa muziki yeye anafanya Amapiano Chino Kidd, alinunua gari aina ya BMW,na pia aliweka wazi kuamia kwenye mjengo mpya.

Agosti 31 mida ya usiku ndipo CEO wa Pluto Republic na Producer wa muziki S2kizzy akasema ameongeza gari kwenye parking yake na gari yenyewe ni Range Rover.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *