Stori kubwa huko mamtoni ni juu ya mwanadada Lori Harvey (26), ambaye ni mtoto wa Steve Harvey, kudaiwa kutemana na muigizaji Damson Idris, ambaye alilithi mikoba ya mahusiano kati yao kutoka kwa Michael B. Jordan.
Kwa mujibu wa mtandao wa The Hollyhood Reporter inalezwa kuwa wawili hao ambao wamedumu takribani miezi 12 wameachana na sasa watabaki kuwa kama marafiki tu.

Na hii ndio orodha ya mastaa ambao mrembo huyo amewahi kuwa nao kwenye mahusiano:-Damson Idris -2023,Michael B. Jordan Novemba :2020 -2022, Abou ‘Bu’ Thiam -: Oktoba 2020, Future :- 2019, Sean ‘Diddy’ Combs :Julai 2019-Oktoba 2019, Trey Songz :2018 – 2019,Lewis Hamilton:- 2019
na Memphis Depay :- Januari 2016 – Juni 2017. Wajuzi wa mambo wanakuabia binti haachwi huyu bali anakuacha.