MASHEIKH WATAKA LAKI 1 ILI KUMSWALIA MAREHEMU, WANANCHI WAPINGA

Vuta nikuvute kwa wakazi wa Kijiji cha Mtakumbuka kilichopo Kata ya Magamba Manispaa ya Mpanda, baada ya Masheikh kuwagomea Wafiwa wa kijiji hicho kuusomea dua mwili wa dereva bodaboda wakitaka ndugu wa marehemu kulipa shilingi laki moja kwanza.

Masheikh hao, (Majina yanahifadhiwa) walisema kiasi hicho cha pesa kinatakiwa kilipwe, ili waweze kumswalia marehemu kwa madai ni fidia yake ya kutofanya ibada enzi za uhai wake.

Wakizungumzia tukio hilo mashuhuda wamedai kuwa mbali na kiasi hicho cha pesa kilichoombwa kama fidia pia inadaiawa kuwa enzi za uhai wake marehemu hakuwa na utaratibu wa kufunga, kufanya ibada, kutoa michango sehemu za ibada na akituhumiwa kuwa alikuwa akinywa pombe.

Hata hivyo, viongozi hao wa dini waliingilia kati suala hilo na kuendelea na taratibu za mazishi ili kumuhifadhi marehemu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *