Mashambulizi ya Israel yaua Wapalestina 13

Israel imesema wanajeshi wake wamewaua magaidi 10 na kuwakamata wanane katika kambi ya wakimbizi ya Nur Shams,wapalestina wasiopungua 13 waliuawa katika shambulio lililofanywa na vikosi vya Israel katika eneo linalokaliwa kimabavu la Ukingo wa Magharibi.

Kundi la wanamgambo la Islamic Jihad limesema wanachama wake watatu waliuawa katika kipindi ambacho Kundi la Tulkarm Brigades, ambalo linajumuisha vikosi kutoka makundi tofauti ya Wa-palestina, limesema wapiganaji wake walipambana kwa silaha na vikosi vya Israel siku ya Jumamosi.

Waandishi wa shirika la habari la AFP wamesema walisikia milio ya risasi kabla ya kuona  miili ikiwa imelala barabarani na nyumba zilizoharibiwa na ndege zisizo na rubani za Israel na jeshi la Israel limesema mapigano hayo yalidumu kwa zaidi ya saa 40 na kwamba wanajeshi wake wanane na afisa mmoja wa polisi walijeruhiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *