MASHAHIDI WA KUFICHWA: MAHAKAMA YATUPILIA MBALI OMBI LA LISSU, CHADEMA KUKATA RUFAA

Kesi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri kuhusu mashahidi kufichwa katika kesi ya kuchapisha taarifa za uongo inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupiliwa mbali.

Uamuzi huo umetolewa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam hii leo Agosti 12, 2025 na Jaji Elizabeth Mkwizu aliyesema uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, uliotolewa na Hakimu Geofrey Mhini kuhusu mashahidi wa Serikali ambao sio raia kutoa ushahidi kwa kificho ulikuwa sahihi.

Lissu alikuwa akiiomba mahakama itengue uamuzi huo, ili ushahidi utolewe na wahusika katika hali ya kawaida wakiwa wanaonekana.

Katika hatua nyingine, CHADEMA imepanga kukata rufaa kupinga maamuzi ya Mahakama Kuu Masijala Ndogo, Dar es Salaam wa kutupilia mbali maombi hayo ya Lissu.

Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema CHADEMA kutoridhishwa kwa chama hicho na uamuzi huo wa Mahakama ambapo amesema amesema si sahihi na kubainisha kuwa chama kitapanga kushauriana na Lissu ili kuwasilisha rufaa kupinga uamuzi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *