Kamati imewafungia kwa miezi sita (6) kuingia viwanjani kwenye michezo ya
michuano yote ya TFF, mashabiki wanne walioonekana kupitia video kwenye
mitandao ya kijamii wakimshambulia shabiki mmoja aliyekuwa amevaa jezi
ya klabu ya Yanga katika mchezo tajwa hapo juu.

Mashabiki hao ni Hassan Khatibu, Hamza Dafa, Patrick Shelukindo na Shaban
Anga. Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 47:2 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa
Klabu.
Bodi imewataka mashabiki kujiepusha na vitendo vya vurugu na kupigana
viwanjani ili kudumisha upendo na umoja michezoni.


