Mashabiki wa Yanga watalipa Milioni 1 ya Ali Kamwe

Baada ya hapo jana Meneja wa ldara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Ali Kamwe kutozwa faini ya Milioni 1 kwa kosa la kumkejeli na kumdhalilisha mwamuzi aliyechezesha mchezo kati ya Singida F.G dhidi ya Simba SC, Tatu Malogo kupitia mitandao yake ya kijamii, kwa kuweka wimbo wa ‘Maokoto’ wa Billnass ft Marioo na picha ya mwanadada huyo.

Hatimaye mashabiki wa Yanga wameweka wazi kumlipia Msemaji wao ambapo Alikamwe amesema amepokea adhabu hiyo kama njia ya Mungu kutaka kuzungumza naye, kwani kupitia adhabu hiyo ameona, kusikia na kujifunza mengi, kikubwa ameuona upendo wa dhati ya mashabiki wa Yanga kwake na amewashukurukwa kuweza kumchangia kiasi hicho cha pesa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *