Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Marufuku wajawazito kwenda na wenza wao kliniki

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, amepiga marufuku wauguzi wa afya kuwataka wajawazito kwenda na wenzao wao kliniki kwa ajili ya kupata huduma za afya.

Kauli hiyo ameitoa leo Novemba 30, 2023, wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia lviwanja vya Jitegemee wilayani Muheza.

Amesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wajawazito kutakiwa kwenda na wenzao wao cliniki ndio watapewa huduma.

“Napiga marufuku wajawazito kuambatana na wenza wao kliniki, bali wapeni elimu juu ya umuhimu wa kujua afya ya mwenza wake na sio kumshinikiza, kwani huo ni sehemu ya ukatili, “amesema Waziri Ummy.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *