MARUFUKU MATUMIZI YA ‘CHAINSAW’ BILA KIBALI – KATAMBI

Na Gideon Gregory – Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) amepiga marufuku matumizi ya Chainsaw bila kibali halali kutoka mamlaka zilizopo katika maeneo hayo hasa Halmashauri. 

Katambi ameyasema hayo leo Mei 5,2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Moshi Vijijini Prof. Patrick Ndakidemi aliyetaka kujua Serikali inatoa tamko gani kuhusu ujangili wa kutumia chainsaw katika kuharibu miti ya asili ambayo inatunza vyanzo vya maji.

“Kwanza pamoja na kwamba mashine hizo zinauzwa hapa nchini lakini kuna utaratibu maalum ambao upo kwaajili ya muongozo kwamba zisitumike hovyo kwenye maeneo ambayo hayajapewa kibari na matumizi yoyote ya chainsaw si tu kwa Kilimanjaro ni nchi nzima,”amesema. 

Aidha, amesema kuwa hata kwa maeneo ya misitu ambayo ipo kwa mujibu wa sheria na inatumbulika kwenye maeneo mbalimbali nako zipo taratibu za kuweza kutumia mashine hizo na namna ya uvunaji kuna utaratibu maalum.

“Kwahiyo nitoe maelekezo kwamba ni muhimu wazingatie utaratibu uliowekwa kikanuni na kisheria katika matumizi ya Chainsaw na kama atakiuka mtu tutachukua hatua kali sana za kisheria kupitia Mamlaka za Mikoa katika wilaya, amesema. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *