Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema tayari bunge limepitisha Sheria ya Udhibiti wa Tumbaku ijulikanayo kama “The Tobacco Products (Regulation) Act, 2003” ambayo imetoa katazo la uvutaji wa Sigara hadharani.
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amebainisha hayo leo Aprili 30,2024 Jijini Dodoma wakati akijibu swali Namba 215 kutoka kwa Mbunge wa Tumbe, Mhe. Amour Khamis Mbarouk aliyeuliza Je, ni lini Serikali italeta Sheria ya Kuzuia uvutaji wa sigara na mazao mengine hadharani.
Aidha amesema sheria hiyo imezuia matangazo ya tumbaku na bidhaa zitokanazo na tumbaku kwenye maeneo ya umma ikiwemo vyombo vya habari, billboards na kwenye matamasha mbalimbali.
Vile vile Dkt. Mollel ametoa wito kwa wabunge kuwa mabalozi wa Udhibiti wa Tumbaku katika jamii ili kusaidia wananchi kuepuka magonjwa yasiyoyakuambukiza
Sheria ya Bidhaa za Tumbaku (Na. 2 ya 2003) ni Sheria ya kudhibiti utengenezaji, usambazaji wa lebo, uuzaji, matumizi, utangazaji wa bidhaa za tumbaku, uvutaji sigara katika maeneo maalum na mambo yanayohusiana nayo.
Contact Us
P. O. BOX 71, Shinyanga, Tanzania
+255 766 408 253
info@jambofm.co.tz