Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Marufuku kuvaa kimini na kunyoa ‘kiduku’

Kata ya Kimnyaki wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha chini ya uongozi wa Kijiji cha Olevolosi,
umeweka sheria ndogo mbalimbali na kupitishwa na mkutano mkuu wa kijiji. Na Mmiongoni mwa yaliyopitishwa ni pamoja na kupiga marufuku wasichana au wanawake kuvaa suruali za kubana au sketi fupi ‘vimini’, na kijana wa kiume kusuka nywele au kunyoa pembezoni mwa kichwa na kuacha nywele katikati ‘kiduku’, kuvaa hereni au kuvaa suruali inayoonyesha makalio na adhabu za makosa hayo ni faini Sh50,000.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa kijiji hicho, Mtendaji wa Kata hiyo ya Kimnyak, Joshua Mollel, aliwasilisha sheria hizo kwa niaba ya mtendaji wa kijiji hicho, ambazo zilipitishwa na mkutano huo.

Sheria nyingine ni kupiga marufuku kijana wa kiume kuvalia hereni, marufuku kijana mwenye nguvu kutokufanya kazi na atakayeonekana kijiweni asubuhi bila kufanya kazi atatozwa faini Sh50,000, ni kosa kupika au kuuza pombe haramu ya gongo na adhabu yake ni kupelekwa mahakamani na atakayekutwa na anauza pombe muda wa kazi atatoza faini Sh50,000.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *