Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Marekani Yaizuia Palestina Uanachama UN

 Azimio la kuungwa mkono uanachama kamili wa taifa la Palestina ndani ya Umoja wa Mataifa limeshindwa kupitishwa kwenye Baraza la Usalama la Umoja huo kufuatia kura ya turufu iliopigwa na Marekani.

Kura ya turufu ya Marekani, ambayo ni mwanachama wa kudumu wa chombo hicho chenye nguvu zaidi ndani ya Umoja wa Mataifa imemaanisha kuwa rasimu ya azimio hilo imeshindwa kupitishwa.

Ili kufanikiwa kwa azimio hilo linahitaji kupigiwa kura na wanachama 9 kati ya 15 wa Baraza la Usalama na kuwepo na kura ya turufu kutoka kwa mwananchama yeyote kati ya watano wa kudumu wa Baraza hilo – China, Ufaransa, Urusi, Uingereza na Marekani.

Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeulaani uamuzi huo wa Marekani na kuutaja kuwa ni uchokozi unaoisukuma mashariki ya Kati kuelekea shimoni,nchi 12 zilipiga kura ya kuunga mkono azimio hilo huku Uswisi na Uingereza zikijizuia.

Balozi wa Israel Umoja wa Mataifa Gilad Erdann akionesha picha mbele ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa namna Iran ilivyoendesha mashambulizi yake.

Mapema mwezi Aprili, Balozi wa Palestina wa Umoja wa Mataifa, Riyad Mansour, alimwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutterres akiomba hoja hiyo, ambayo tayari iliwasilishwa mwaka 2011, lakini haikuweza kupitishwa iwasilishwe tena kwa Baraza la Usalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *