Marekani yahofia RSF kushambulia El-Fashir Sudan

Afisa mwandamizi wa Serikali ya Marekani Linda Thomas-Greenfield ameonya kwamba zaidi ya watu milioni 2 katika mji wa El Fashir jimbo la Darfur Magharibi mwa Sudan, wako chini ya tishio la mauaji makubwa kutokana na shambulio linalotarajiwa la kundi la wanamgambo la RSF.

 “Tayari kuna ripoti za kuaminika kwamba RSF na wanamgambo washirika wake, wameharibu vijiji vingi magharibi mwa El Fasher,” Balozi Thomas-Greenfield amewaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

RSF ni Kikosi kinachotawaliwa ni kikundi cha wanamgambo ambacho kinaundwa na wapiganaji wa Janjaweed ambao walifanya mauaji ya halaiki huko Darfur katika miaka ya 2000 na Mkuu wa kikundi hicho amekuwa kwenye mvutano wa kuwania madaraka kwa kutumia silaha na mkuu wa jeshi la Sudan kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Mapigano hayo yameenea kutoka mji mkuu wa Sudan, Khartoum, hadi maeneo mengine ya nchi, na sasa yanaonekana kuwa tayari kuikumba Darfur Kaskazini na raia walionaswa huko na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana ili kujadili hali hiyo na limepokea taarifa kutoka kwa maafisa wa Umoja wa Mataifa wa kisiasa na kibinadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *