Cynthia Omowumi Aloba, mke wa marehemu Mohbad, ameweka wazi kutokuwa na mahusiano mazuri na baba wa Mohbad.
Mrembo huyo anasema kuwa babake Mohbad anaamini kwamba yeye ni chanzo cha kutengana na kijana wake kwani tangu wapate mtoto wao Liam uhusiano kati yao ulipoteaa
Cynthia amefunguka hayo jana wakati wa kutoa ushahidi wake katika Mahakama ya Candide-Johnson House iliyopo Ita-Elewa, Ikorodu, ambapo pia alieleza kuwa anapokea vitisho vya kutaka kuuliwa tangu mumewe huyo afariki.
