MAPINDUZI CUP SASA NI TIMU ZA TAIFA TU SIO VILABU TENA…

Mashindao ya Kombe la Mapinduzi yanatarajiwa kuanza kuchezwa Januari 03 2025 na fainali inategemewa kuchezwa Januari 13 2025 ambapo Kamati ya mashindano ya kombe la Mapinduzi kupitia Makamo Mwenyekiti wake ndugu Suleiman Jabir rasmi yatoa muongozo mpya wa mashindano hayo.

Mfumo wa mashindano hayo kwa msimu 2025 utajumuisha timu za taifa badala ya timu za vilabu hii ni kufuatia Tanzania, Kenya na Uganda kuwa wenyeji wa mashindano ya Afcon na CHAN na kutoa fursa ya kupata mazoezi kwa timu za Taifa.

kabla ya hapo kutakua na droo maalum ya kupanga makundi ya mashindano hayo na mashindano hayo kwa msimu huu yatafanyika katika uwanja wa Gombani Pemba badalaya uwanja wa Amaan ambao uko kwenye maboresho

Timu za taifa zinazotarajiwa kushiriki Mapinduzi Cup ni pamoja na Zanzibar Heroes, Kenya, Uganda, Kilimanjaro Stars, Burundi na Burkina faso .

Mshindi anatarajiwa kupata kiasi cha Shilingi Milioni Mia moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *