
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinaadamu inasema raia nchini Sudan wamenasa kwenye ukatili usioelezeka unaosababishwa na mapigano huku janga la njaa na maradhi yakichanganyika na maafa hayo.
Afisa wa ngazi za juu wa ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa, Clementine Nkweta-Salami, aliwaambia waandishi wa habari jijini New York siku ya Jumatano (Mei 15) kwamba ukatili wa kutisha unatendwa kwa raia wasiokuwa na hatia.
Msemaji huyo amesema kuna ripoti za ubakaji, mateso na mauaji yenye misingi ya kikabila Aidha Mapema mwezi huu, Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa lilizionya pande zinazonpigana nchini Sudan kwamba kuna hatari kubwa ya vifo vinavyotokana na njaa ndani ya jimbo la Darfur na pia maeneo mengine ya nchi hiyoo, endapo hawakuruhusu misaada kulifikia eneo zima la magharibi mwa nchi.
Kwa mujibu wa Nkweta-Salami, mapigano makali yalishuhudiwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mji huo wenye wakaazi 800,000 na kusababisha vifo kadhaa na kuwakimbiza watu kutoka makaazi yao, Katikati ya mwezi Aprili, wafadhili waliahidi msaada wa dola bilioni 2.1 kati ya bilioni 2.7 zilizoombwa na Umoja wa Mataifa, lakini hadi kufikia sasa fedha zilizotolewa ni asilimia 12 ya kiwango hicho.


