MAPENDEKEZO: KWENDA NA WAGOMBEA WATATU SI BUSARA – DKT. SAMIA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasilisha mapendekezo katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ya kurekebisha katiba ya chama, ili kuruhusu kuongezwa kwa idadi ya wagombea wanaopitishwa kutoka watatu hadi kufikia wanne au watano, kulingana na uhitaji.

Wasilisho hilo lililotolewa hii leo Julai 26, 2025, linalenga kukabiliana na changamoto ya ongezeko kubwa la wanachama wa CCM wanaowania nafasi za uongozi katika ngazi mbalimbali, kufuatia uamuzi wa chama wa kupanua demokrasia ya mchakato wa uteuzi.

Katika Mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao, Dkt. Samia amesema baadhi ya majimbo yamekuwa na hadi wagombea 39 hadi 40, hivyo si busara kuchukua majina matatu pekee.

Amesema, “mtakumbuka tuliamua kupanua demokrasia katika uteuzi wa viongozi kuanzia ngazi ya taifa, jimbo hadi kata. Hatua hii imevutia wanachama wengi zaidi kuwania nafasi. Hivyo, tumeona kuwa kuchuja wagombea watatu tu kutoka kundi kubwa kama hilo si sahihi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *