Watoto wawili ambao ni Mapacha wenye umri wa miaka 17 Wakazi wa Kijiji cha Bubale kilichopo Kata ya Nkololo Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu wamefariki dunia baada ya kupewa dawa na mganga wa tiba asili kwa lengo la kuwaongezea matiti ili waweze kuolewa.
Majirani waishio karibu na mganga huyo akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Byuna wamessma mganga huyo anaitwa Masunga Tumolo na wamekiri kuwa Watoto hao walikuwa kwa mganga huyo Kijiji cha Byuna ambako walikwenda kuoga dawa ya kuwaotesha matiti.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Byuna, Dkt. Deogratius Mtaki amesema awali alipokea mwili wa Dotto na baadae akampokea Kulwa akiwa mahututi baada ya muda mfupi naye akapoteza uhai.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga amefika eneo la tukio ambapo amekemea kitendo hicho na kulitaka Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na tukio la mauaji ya Mabinti hao.