Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Maofisa 575 watunukiwa  kamisheni

Rais wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amewatunuku kamisheni kwa cheo cha luteni usu maofisa 575 kati yao wanawake ni 93 na wanaume 482 huku 62 wakitunukiwa shahada ya kwanza ya sayansi ya kijeshi.

Mahafali hayo ya nne yamefanyika katika chuo cha kijeshi Monduli Mkoani Arusha ambapo Rais Samia pamoja na mambo mengine amekagua gwaride maalum na kutunuku kamisheni kwa wahitimu.

Mkuu wa chuo hicho Brigedia Jenerali Jackson Charles Mwaseba ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia kwa kukubali kutoa kamisheni hiyo na kutoa mchanganuo wa kitaaluma.

Aidha, Waziri wa Mambo ya Ndani na Kaimu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhandisi Hamad Masauni amesema chuo kinaendelea kufanya juhudi mahususi katika kuboresha mitaala ya mafunzo ili kupata wahitimu wenye uwezo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *