Na Saulo Stephen – Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ya Mkoani Singida, Dkt. Vicent Mashinji amesema Wilaya hiyo ipo tayari kushiriki zoezi la upigaji kura katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29, 2025 na kusisitiza kuwa hali ya amani ipo vizuri Wilayani humo.
DC Mashinji ameyabainisha hayo hii leo Oktoba 22, 2025 wakati akizungumzia hali ya usalama na amani katika Wilaya ya Manyoni katika kipindi hiki cha kuelekea siku ya Uchaguzi Mkuu na baada, ambapo amesema wamejipanga vyema kuhakikisha Wananchi wa Wilaya ya Manyoni wanapiga kura kwa amani na utulivu.

Aidha, ametoa wito kwa wakazi wa Wilaya hiyo kujitokeza kwenye vituo vya kupigia kura kwani serikali ya Wilaya hiyo itahakikisha kila mtu anapinga kura kwa amani na usalama.
Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 ambapo kila Mtanzania mwenye sifa atashiriki kuchagua Kiongozi katika ngazi za Udiwani, Ubunge pamoja na Uais.


