Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) yaimarisha udhibiti wa uingizwaji wa dawa holela nchini

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa Magharibi imesema imeimarisha zaidi udhibiti wa uingizwaji wa dawa holela ambazo hazijasajiliwa ama kutolewa kibari maalum ili kuingiza nchini kupitia mipaka rasmi na isiyo rasmi kwa lengo la kudhibiti dawa hizo ambazo zikitumiwa na wananchi zinaweza kuleta madhara makubwa ya kiafya kwa watumiaji.

Hayo yamebainishwa na Mkaguzi wa Dawa kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa Magharibi Venance Burushi wakati akizungumza na Jambo Fm katika ofisi za makao makuu ya TMDA kanda ya ziwa zilizopo mjini Geita ambapo amesema mamlaka hiyo imeweka wakaguzi kwenye mipaka rasmi ili kudhibiti dawa hizo na ambazo zimeingizwa kupitia mipaka isiyo rasmi pamoja na kufanya ukaguzi kwenye maduka ya dawa na hospitali binafisi ili kuzibaini dawa hizo.

Aidha Venance amesema kutokana na wananchi wengi kuwa na mazoea ya kununua na kutumia dawa kiholela bila kufahamu wanasumbuliwa na ugonjwa gani hali hiyo imekuwa ikizalisha magojwa makubwa ambayo kuyatibu imekuwa ni changamoto hivyo mamlaka hiyo imewataka wananchi kutumia dawa kwa kuzingatia maelekezo ya wataalam wa afya ili kuepukana na wimbi hilo la matumizi holela ya dawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *