Mamlaka ya Kitaifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya Nigeria (NDLEA), imetoa ufafanuzi wake juu ya picha iliyowekwa mtandaoni na Naira Marley akiwa kwenye ofisi hizo na kusema kuwa sio kama wamemteua kuwa balozi wa Mamlaka hiyo .

Msemaji wa taasisi hiyo, Bwn. Femi Babafemi amefafanua kuwa msanii huyo akiongozana na timu yake walifanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Shirika hilo, kujionea namna wanavyofanya kazi na aliweka wazi kuwa tayari a kujiunga na vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya nchini humo, na kubainisha kutumia sanaa yake kuweka maudhui yatayoonja watu kutumia madawa ya kulevya.