Mambo ni fresh kituo cha afya Kambarage

Serikali imetumia zaidi ya shilingi milioni 500 kutekeleza mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje,jengo la wagonjwa wa ndani,jengo la mionzi na njia za waenda kwa miguu katika kituo cha Afya Kambarage kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga.


Hayo yamebainishwa Julai 28,2023 kupitia ripoti iliyosomwa mbele ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Bw.Abdalla Shaib Kaim kabla ya Kuzindua Mradi huo ambao ameelezea kuridhishwa na utekelezaji wake.
Sehemu ya taarifa kuhusiana na utekelezaji wa Mradi huo imeeleza kwamba awali serikali ilitoa Shilingi milioni 500 kwa lengo la Ujenzi wa hospitali mpya ya Manispaa ya Shinyanga kabla ya Katibu mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi kuahirisha matumizi ya fedha hizo na kuzielekeza katika kituo cha Afya Kambarage kwaajili ya maboresho ya Miundombinu.


Hatua hiyo ilikuja kufuatia Manispaa ya Shinyanga kukabidhiwa iliyokuwa hospitali ya Mkoa ambayo kwasasa ni hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.


Ukiwa ndani ya Halmashauri ya Shinyanga mwenge wa Uhuru umepitia na kufanya shughuli za uwekaji wa mawe ya msingi,kufungua,kuzindua na kuona jumla ya miradi kumi(10)ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi za Kitanzania 2,078,353124.40

Comments are closed.