Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe amesema klabu hiyo haitokuwa tayari kucheza mechi dhidi ya Simba SC uliopangwa Juni 15, 2025 ikiwa kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Bodi ya Ligi haitovunjwa, na Afisa Mtendaji wa Bodi hiyo kujiuzulu.
Akizungumza hii leo Juni 9, 2025 jiiini Dar es Salaam, Kamwe amesema, “tumepeleka matakwa yetu kwa Bodi ya ligi na kama ikiwa hayatafuatwa huu ndio msimamo wetu, hatuta cheza mchezo wa Dabi, hatutacheza mechi zilizobakia za ligi wala hatutashiriki ligi kuu msimu ujao.”

“Tumetoa matakwa manne. Matatu yanahusu mchezo namba 184, tunaamini yakifanyiwa kazi hayo matatu kwanza, tutakuwa tayari kucheza mechi hiyo kwa tarehe nyingine itakayopangwa. Na takwa la nne ni la muda mrefu, kuanzia msimu ujao. CEO wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo asiudanganye UMMA kwa kuchagua kuzungumzia takwa moja tu na kuacha yanayotakiwa kushughulikiwa kwa haraka ikiwemo yeye mwenyewe kujiuzulu,” aliongeza Ally Kamwe.
Tayari Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Almas Kasongo amethibitisha kupokea maazimio manne ya Yanga SC yaliyowasilishwa leo, huku akidai kiwa wanafanyia kazi yale yaliyoko ndani ya uwezo wao.