Mama Mohbad alia akitaka Naira Marley akamatwe

Mama mzazi wa Mohbad, Bi Promise Aloba, amewataka viongozi wa Nigeria, kuhakikisha wanamtia nguvuni msanii Naira Marley.

Bi Aloba ametoa kauli hiyo baada ya uongozi wa serikali kufika kwake kwaajili ya kumpa mkono wa pole ambapo waliongozwa na Seneta Ndg: Elisha Abbo, ambaye aliambatana na waigizaji wa Nollywood, Bi. Tonto Dikeh na Bi. Iyabo Ojo.

“Najua mwanangu; aliniambia kuwa Naira Marley huwa anamtishia maisha yake sana. Naombeni sanaa Wanigeria, nisaidie kumtafuta; tafadhali nihurumie; hiyo ndiyo tu unaweza kunifanyia jamani,” alisema mama huyo kwa uchungu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *