Staa wa filamu ya Breaking Bad, iliyotoka 2008 na kumalizika 2013 Aaron Paul amefunguka kutopata pesa yoyote/Mirabaha ya filamu hiyo kupitia mtandao wa Netfix ambao wanaonesha filamu.
Paul pamoja na waigizaji wenzake wa filamu hiyo, Bryan Cranston, Jesse Plemons na waigizaji wenzao wameingia katika Mgomo wakidai malipo ya kazi zao zinazooneshwa kwenye Netfix.
“Sipati mirabaha yangu kutoka kwa Netflix kwenye ‘Breaking Bad’ huu ni wazimu kwangu,” amesema Paul akizungumza na mwandishi.