Mataifa ya Burkina Faso, Mali na Niger yamejivua uanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), kwa madai kuwa mahakama hiyo inaendekeza ukoloni mamboleo na ubaguzi katika hukumu zake.
Mataifa hayo, yamedai ICC imekuwa ikiwaandama viongozi kutoka mataifa masikini na kutowahukumu wanaofanya uhalifu mbaya zaidi ulimwenguni.

ICC inashutumiwa kwa kushindwa kushughulikia kesi za uhalifu wa kivita na mauaji makubwa na badala yake kutumiwa kuwalenga watu binafsi.
Hata hivyo, nchi hizo zimesema uamuzi wa kujiondoa ni njia ya kulinda uhuru wao wa kitaifa na wataimarisha mifumo ya ndani ya haki na amani inayozingatia maadili ya kijamii.


