Katibu wa,itikadi, uenezi wa chama cha mapinduzi Paul Makonda amewataka viongozi wa serikali mkoani Simiyu kusitisha mara moja mipango ya matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani na badala yake wawaache wakulima wenyewe wachague ni nani wanayetaka kumuuzia mazao yao.
Agizo hilo la Makonda limekuja kufuatia ombi la mbunge wa jimbo la bariadi na naibu waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari mhandisi Kundo Mathew ambaye aliomba wakulima waruhusiwe kuuza mazao yao kwa wafanyabiashara wanaowataka wao badala ya kulazimishwa kutumia mfumo huo