Makonda amesema hajaja kulipa kisasi kwa yeyote

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Paul Makonda amesema tangu ateuliwe kuna Watu wamehamaki wengi wao wakiwaza kuwa Makonda atalipiza kisasi huku wengine wakiwataja baadhi ya Watu na kuwaambia ‘Utaona sasa usiyemtaka kaja’, ambapo Makonda amesema hajaja kulipa kisasi kwa yeyote.

“Tangu niteuliwe nimepata nafasi ya kupitapita kwenye mitandao nimesoma maoni ya baadhi ya watu, wengi wanahamaki na wengi wanabashasha, na waonaohamaki wengi wao wanawaza tu Makonda ataenda kulipa kisasi, wanawaza Makonda ataenda kufanya nini, wengine wameanza kuwataja wengine kwamba utaona sasa, unayemtaka kaja, mimi niseme sina kisasi kwa mtu yeyote,” -Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Paul Makonda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *