Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM taifa (NEC) Itikadi,Uenezi na Mafunzi Paul Makonda amefanya maombi na mjane wa Hayati Dkt John Pombe Magufuli, Janeth Magufuli alipomtembelea nyumbani kwake Chato mkoani Geita.
Makonda amemtembelea mjane huyo pamoja na kuzuru kaburi la Hayati Magufuli jana Ijumaa Novemba 10, 2023 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa Kagera, Geita, Mwanza,Mara, akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa idara yake ya uenezi CCM Taifa.