Makonda aanza kazi, atoa miezi sita

Chama cha Mapinduzi CCM, kimemtaka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ndani ya miezi sita awe amesimamia kikamilifu kuondoa na kufuta migogoro yote ya ardhi inayopelekea wavuvi, wakulima, wafugaji na wananchi kuteseka.

Maagizo hayo yametolewa na katibu wa NEC, itikadi na uenezi Paul Makonda wakati akizungumza na wakazi wa Dodoma katika mkutano wa hadhara baada ya kupokelewa.

Aidha ameongeza kuwa chama kimetoa miezi miwili kwa waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Jerry Silaa kuhakikisha anatatua migogoro ya ardhi iliyopo mkoani Dodoma.

Awali akizungumza na wananchi katika mkutano huo waziri wa madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Antony Mavunde amesema watahakikisha wanaendelea kutatua kero za wananchi kwa mujibu wa ilani ya chama hicho.

Kwa kuwa Chama hicho kimejiwekea utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi Makonda ametoa fursa kwa wananchi kueleza kero zao na kuziwasilisha kwa wahusika ili kupatiwa ufumbuzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *