Makamu Wa Rais, Dkt. Philip Mpango Anatarajia Kuwa Mgeni Rasmi Katika Uzinduzi Wa Maonesho Ya Miaka 60 Ya Jeshi La Kujenga Taifa (JKT).
Taarifa Hiyo Imetolewa Leo Na Waziri Wa Ulinzi Na Jeshi La Kujenga Taifa (JKT), Alipotembelea Maandalizi Ya Maonesho Hayo, Huku Akilipongeza Jeshi Hilo Kwa Maandalizi Mazuri Waliofanya.
“Nawapongeza Sana Kwa Hiki Mlichokifanya, Tulianza Na JKT Marathon Ambayo Ilifana Sana Na Hivi Sasa Maonyesho Ya JKT Ambayo Yanajumuisha Vitu Mbalimbali” Amesema Bashungwa.
Waziri Bashungwa Amesema Hii Inaonyesha Jinsi Gani Jeshi Hilo Lilivyojipanga Kusherekea Maadhimisho Ya Miaka 60 Toka Kuanzishwa Kwake Ikiwemo Kuonyesha Kazi Mbalimbali Inazofanya.