MAKAMU WA RAIS AUTAKA URAIS WA ZANZIBAR….

Mwenyekiti Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mh. Othman Masoud Othman ametangaza nia ya kutaka kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar 2025 kama chama chake kitampitisha.

Mh. Othman amefikia Uamuzi huo leo na kutangaza nia hiyo huku akisema itakapofika wakati wa kuanza mchakato wa kutafuta wagombea katika chama hicho kwa ajili ya uchaguzi wa 2025 amekusudia kukiomba chama chake cha ACT Wazalendo kumpa dhamana ya kuiwakilisha kwenye nafasi ya uongozi wa juu wa Urais wa Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *