Makamu Wa Rais Dkt. Philip Mpango Ametoa Wito Kwa Wajawazito Kuhakikisha Wanahudhuria Kliniki Wakati Wote Wa Ujauzito Ili Kutambua Mapema Hatari Zinazoweza Kujitokeza.
Makamu Wa Rais Amesema Hayo Wakati Wa Makabidhiano Ya Vifaa Tiba Kwa Ajili Ya Watoto Wanaozaliwa Kabla Ya Wakati (Njiti) Vilivyotolewa Na Taasisi Ya Doris Mollel Pamoja Na Vifaa Tiba Vilivyotolewa Na Tume Ya Ushindani (FCC) Katika Hospitali Ya Wilaya Ya Buhigwe Mkoani Kigoma.
Pia, Amekemea Tabia Za Ukatili Hususani Kuwapiga Wajawazito, Na Kusema Kuwa Madhara Yake Ni Makubwa.
Makamu Wa Rais Ametoa Rai Kwa Viongozi Wa Dini, Serikali Na Kisiasa Kushirikiana Katika Kuwachukulia Hatua Wale Wote Wanaofanya Ukatili Kwa Wajawazito.
Amewataka Watanzania Kuachana Na Tabia Za Kuwapa Msongo Wa Mawazo Wajawazito, Kwani Ni Moja Ya Sababu Zinazopelekea Changamoto Za Uzazi Ikiwemo Kujifungua Mtoto Kabla Ya Wakati (Njiti).
Dkt. Mpango Ameipongeza Taasisi Ya Doris Mollel Ambayo Imekuwa Ikitekeleza Shughuli Zake Kwa Takribani Miaka Nane Katika Kusaidia Serikali Kutoa Huduma Kwa Watoto Waliozaliwa Kabla Ya Wakati Na Pia Kusaidia Katika Utoaji Wa Vifaa Tiba Vinavyotumika Kuokoa Maisha Ya Watoto Hao.