Na William Bundala, Kahama – Shinyanga.
Makampuni 34 yanayofanya kazi katika mgodi wa dhahabu wa Bulyankulu wilayani kahama mkoani shinyanga, yametajwa kukwepa kulipa ushuru wa Huduma ya jamii kitendo ambacho kimekuwa kikipunguza mapato ya ndani ya halmashauri ya Msalala na kukwamisha kasi ya maendeleo.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wa wilaya ya kahahama Mboni Mhita katika kikao maalumu cha baraza la kupitia hoja za mkaguzi wa hesabu za serikali C.A.G Nakuigiza halimashauri kuzichukulia hataua za kisheria baada ya kufanya na mazungumzo na kukaidi makubaliano waliyokuwa wamekubaliana hapo awali.
“Kuna hoja ya makampuni 34 yanayoyofanya kazi kwenye Mgodi wetu wa Bulyanhulu yanadaiwa ushuru wa huduma za jamii,Huu ushuru siyo hisani ni taratibu za serikali na mikataba walisaini,Sasa halmashauri chukueni hatua za kisheria dhidi ya makapuni hayo mana mliwaita mara ya kwanza ila wamekaidi makubaliano” Amesema Mhita.
Hataa hivyo Mhita amelipongeza baraza kwa kusimamia shughuli mbalimbali za kimaendeleo kwa ushirikiano ambao umepelekea kuwepo kwa hati safi ambayo imetokana na umakini wa usimamizi wa miradi kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
“Hii hati safi ni ishara kuwa usimamizi wa miradi ya mandeleo katika kata zenu umeenda vizuri niwapongeze kwa ushirikiano wenu na kusimamia vyema fedha za miradi ya maendeleo” Amesema Mhita.
Sambamba na hayo halimashauri hiyo bado inahoja 56 ambazo zinatakiwa kufungwa kwa muujibu wa sheria za kihasibu licha ya halmashauri hiyo kuunda kamati ya ufuatiliaji kuhakikisha zinafungwa.
Makamu mwenyekiti na diwani wa kata ya Mwakata Sixberth Mpemba ameiagiza Ofisi ya mkurugenzi mtendaji kusimamia kwa haraka jambo hilo ili hoja hizo ziweze kufungwa.
“Sasa niagize ofisi ya mkurugenzi mtendaji kusimamia kwa haraka jambo hili ili hoja hizi ziweze kufungwa,lakini pia niwashukuru madiwani wenzangu kwa kazi nzuri mlizofanya katika kata zenu hususan kusimamia miradi ya serikali” Amesisitiza Mpemba.
Kwa upande wake mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali mkoa wa Shinyanga Yusuph Mabwe amewataka wataalam na madiwani wa halmashauri ya Msalala kuzingatia hatua za manunuzi ili kupunguza uwepo wa hoja nyingi ambazo zinaleta shida.
“Niwaombe wataalamu na Waheshimiwa madiwani zingatieni taratibu za manunuzi hii itasaidia kupunguza uwepo wa hoja nyingi za C.A.G na kufanya ukaguzi usilete mashaka katika halmashauri yenu” Amesema Mabwe.