MAKAMBALA AWATAKA WATAALAM WA HALMASHAURI MANYONI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO

Na Saulo Stephen – Singida.

Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida, wametakiwa kusimamia miradi ya maendeleo kwa umakini na kuhakikisha inatekelezwa kwa ubora ili kuwanufaisha wananchi na kuleta maendeleo yaliyokusudiwa.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Tano John Makambala, wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Tano John Makambala.

Makambala amesema wataalamu wanapaswa kushirikiana kwa karibu na viongozi pamoja na wananchi katika utekelezaji wa miradi na utoaji wa huduma mbalimbali.

Aidha, amewataka wakuu wa idara na vitengo kuwasikiliza wananchi, kushughulikia changamoto zinazowakabili kwa wakati na kuhakikisha huduma zinaboreshwa.

Mbali na hilo, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya madiwani, wakuu wa idara na vitengo pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali zilizopo Wilayani Manyoni ili kuharakisha maendeleo ya wananchi na halmashauri kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *