Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Makalio na matiti kuongezwa Mloganzila

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa mara ya kwanza nchini itafanya huduma za kibingwa bobezi za upasuaji wa kupunguza uzito na upasuaji rekebishi (Bariatric and Reconstructive surgery) kuanzia tarehe 27.10.2023.

Mkuu wa Idara ya Upasuaji Dkt. Eric Muhumba amesema upasuaji huo utafanywa na wataalamu wa MNH-Mloganzila kwa kushirikiana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa kupunguza uzito na Upasuaji Rekebishi kutoka India, Dkt. Mohit Bhandari pamoja na MedINCREDI .

Dkt. Muhumba ameongeza kuwa huduma hizo za kupunguza uzito zinafanyika kwa kupunguza nafasi ya kuhifadhi chakula kwa kushona sehemu ya eneo la tumbo kitu kitakachosababisha mtu kutumia kiasi kidogo cha chakula hivyo kupunguza uzito.

Dkt. Muhumba amebainisha kuwa katika kutoa huduma hizo watatumia njia ya kisasa ambayo haitahusisha upasuaji ambapo watatumia kifaa maalumu kiitwacho endoskopia kuingia katika tumbo na kupunguza nafasi ya tumbo la chakula.

Sambamba na huduma hizo Dkt. Muhumba ameongeza kuwa huduma rekebishi itahusisha kurekebisha kwa kupunguza mafuta na kurekebisha sehemu ya mwili mfano kupunguza au kuongeza ukubwa wa matiti, nyama kwenye mikono na sehemu nyingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *