MAKADA CHADEMA WAPINGA KUSUSIA UCHAGUZI MKUU

MSIMAMO wa Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), umezidi kupingwa vikali baada ya makada wake ambao pia ni watia nia wa Ubunge kujitokeza hadharani kuupinga, wakisema unaenda kukiweka pabaya chama chao.

Wanachama hao wakiongozwa na Jonh Mrema, Catherine Ruge, Julius Mwita, Susan Kiwanga, Grace Sindato Kiwelu, Daniel Naftari Ngogo, Henry Kilewo na Francis Kishabi, wamesema pia ni uhaini kuzuia uchaguzi mkuu kutofanyika.

Wanachama hao wanaokadiriwa idadi ya watu 55 wameeleza kuwa kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu juu ya harakati za kuzuia uchaguzi kwa kusema “No Reforms, No Elections” haiwezi kukisaidia chama chao.

“Sisi tunaunga mkono msimamo wao wa kuunga mkono juhudi za kutaka mabadiliko, ila lazima tujue kuwa si kazi rahisi kuzuia uchaguzi mkuu tukiwa nje ya mfumo wa uchaguzi mkuu kama anavyojaribu kusema Lissu.

“Uwezekano pekee wa kuzuia uchaguzi ni kushiriki uchaguzi wenyewe kwa kuhakikisha tunaingiza wagombea katika uchaguzi.

Ni rahisi kwa wagombea kuhamasisha na kuongoza wananchi kuzuia uchaguzi katika vituo mahsusi vya uchaguzi, katika kata au majimbo yanayoelekea kufanyiwa hujuma kuliko kujaribu kuzuia uchaguzi wote huku tukiwa nje kabisa ya uchaguzi wenyewe,”Iliendelea kusema taarifa hiyo iliyosainiwa na wanachama 55 waliotia ya kuwania nafasi ya ubunge kupitia Chadema.

Kwa mujibu wa makada hao, Tamko la Mwenyekiti wa Chama Taifa, Tundu Lissu, wakatii anahutubia mkutano wa hadhara mkoani Iringa ametamka wazi kuwa, “wote wanaoona, “No Reforms, No Elections” haiwezekani ni wana-CCM pamoja na vibaraka wao” ni kauli ya kusitikisha na inazuia uhuru wa kutoa maoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *