Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dotto Biteko wamewasili Jijini Arusha kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya aliyekua Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa.

Ibada ya maziko itafanyika Kijiji cha Ngarash, Wilayani Monduli mkoani Arusha. Mazishi hayo yataongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.


