MAJALIWA AZINDUA MFUMO WA KIDIJITALI, ATAKA TAASISI ZOTE ZIJISAJILI KURAHISISHA HUDUMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezinduaa mfumo wa kidijitali, utakaoongeza ufanisi wa kazi katika Sekta ya Utumishi wa Umma, huku akizitaka Taasisi zote kujisajili kweye mifumo hiyo yenye lengo la kurahisisha huduma.

Majaliwa azindua mfumo huo hii leo Juni 23, 2025 katika Viwanja vya Chinangali Park katika kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma aliyoitamatisha kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na makundi mbalimbali ya watu ambao walifika kujionea namna Serikali inavyotoa huduma zake kwa jamii.

Awali Wakili wa Serikali, Catherine Paul alisema wengi wa Wananchi waliotembelea banda la Mwanasheria Mkuu wa Serikali wamekuwa wakitaka kujua kuhusu masuala ya Ardhi, Mirathi na mambo yahusuyo Mikataba.

Wakili wa Serikali, Catherine Paul.

Hitimisho la wiki ya Utumishi wa Umma lilitazamiwa kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan lakini kwa niaba yake kazi hiyo ilihitimishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *