MAJALIWA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI KITAIFA

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amezindua Kampeni ya Kitaifa ya upandaji miti kwa kupanda mti wa asili aina ya Mkangazi (Khaya anthotheca) l, katika Viwanja vya Sabasaba, Halmashauri ya Njombe.

Uzinduzi huu uliofanyika hii leo Machi 21, 2025 ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Siku ya Upandaji Miti Kitaifa, yaiwa na kaulimbiu isemayo “Ongeza Thamani ya Mazao ya Misitu kwa Uendelevu wa Rasilimali za Misitu kwa Kizazi cha Sasa na Kijacho.”

Katika uzinduzi huo, Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania kushiriki kikamilifu uhifadhi wa misitu na kusisitiza umuhimu wa miti kama Mkangazi, inayotumika kwa mbao, dawa, na kuni kwa ustawi wa mazingira na vizazi vijavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *