Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mahrez atimkia Al Ahli ya Saudi Arabia

Nahodha wa timu ya taifa ya Algeria, Riyad Mahrez amekamilisha uhamisho wake kutoka klabu ya Manchester City kwenda Al Ahli inayoshiriki ligi kuu nchini Saudi Arabia, Saudi Pro League.

Mahrez (32) ambaye alikuwa amebakisha miaka miwili kwenye mkataba wake, amejiunga na miamba hiyo kwa dau lenye thamani ya pauni milioni 30.

Manchester City ililipa kiasi cha pauni milioni 60 kumsajili Mahrez mwaka 2018 kutoka Leicester city, ambapo amefunga mabao 15 kwenye michezo 47 msimu uliopita.

Mahrez ameisaidia Manchester City kushinda Mataji 10 katika misimu mitano ya kuitumia klabu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *