Mahakama Yatoa Masaa 48 kwa Madaktari Kenya

Mahakama ya nchini Kenya imewataka madaktari na serikali kufikia makubaliano ya kusitisha mgomo ndani ya saa 48 maandamano yanayopaswa kukoma ifikapo ijumaa ya wiki hii.

Madaktari kutoka hospitali za umma waliitisha mgomo wa nchi nzima kuanzia katikati ya mwezi Machi wakishinikiza malipo zaidi na uboreshwaji wa mazingira ya kazi na hivyo kuathiri huduma za afya nchini Kenya,chanzo cha mzozo huo kikiwa ni hatua ya serikali kupunguza mishahara ya wahudumu wa afya wanaofanya kazi kwa karibu asilimia 30 ya madaktari,  Wafamasia na madaktari wa Meno nchini Kenya.

 Hakimu wa mahakama ya kuu, kitengo cha kazi Byram Ongaya amesema muungano wa kitaifa wa madaktari na serikali lazima waitishe mkutano mara moja bila masharti na kurudi kazini siku ya Ijumaa na kusisitiza kwamba pande zote lazima zijadili kwa nia njema kabisa kuelekea maafikiano na kwa manufaa ya kurejesha huduma za afya kikamilifu na kuutaka Muungano wa Madaktari kuhakikisha kuna idadi maalum ya madaktari katika hospitali zote kushughulikia dharura huku mazungumzo yakiendelea.

Mapema mwezi huu, madaktari hao walikataa ofa ya serikali iliyosema itakidhi baadhi ya matakwa ya matabibu, ikiwa ni pamoja na kuajiri wafanyakazi wa ndani kwa kandarasi za kudumu na kulipa malimbikizo yanayodaiwa chini ya makubaliano ya 2017.

Gazeti la Daily Nation siku ya chini Kenya jana liliripoti kuwa mvutano huo umesababisha vifo vingi, na hakuna wataalam katika baadhi ya hospitali zinazotoa matibabu ya saratani,Mamia ya wagonjwa sasa wameweka maisha yao rehani katika katika hospitali za kibinafsi na zahanati za vijijini, ilisema.Mnamo 2017, madaktari walifanya mgomo wa siku 100 nchini kote ambao uliacha hospitali za umma zimefungwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *