Ombi la upande wa mashtaka la kutaka kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kusikilizwa kwa njia ya mtandano limekataliwa na Mahakama.
Uamuzi huo umetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hii leo Mei 6, 2025 jijini Dar es Salaam na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Geoffrey Mhini.

Amesema, “kwa misingi ya utoaji haki, naelekeza mshtakiwa huyu tarehe ijayo aletwe Mahakama ya Kisutu ili aweze kusikiliza kesi yake kwa njia ya kawaida.”
Kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi na badala yake sasa wamekubaliana na upande wa utetezi kutaka Mshtakiwa huyo apelekwe Mahakamani, ili kusikiliza kesi yake.