Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam leo Februari 23 imemuacha huru mke wa marehemu Bilionea Erasto Msuya, Bi. Miriam Mrita pamoja na mfanyabiashara Revocatus Everest baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa dhidi yao.
Bi Mariam Mrita na Revocatus Ernest walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mwaka 2017 wakikabiliwa na kesi ya jinai namba 103 wakituhumiwa kumuua mdogo wa bilionea Msuya, Aneth Msuya kwa kumchinja Kigamboni, Mei 26, 2016.