MAHAKAMA: BESIGYE ANA HALI MBAYA, WANAHARAKATI WAONYA

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye amefikishwa katika Mahakama ya kiraia, ambapo Mawakili wake walijaribu kumpambania ili aweze kuachiliwa, huku Hakimu akisema mtuhumiwa huyo ana hali mbaya.

Besigye ambaye yuponkizuinixi tangu Novemba 2024, akiwa Mahakamani hapo ameonekana kudhoofika na alirudishwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali lililopo jijini Kampala.

Kuzuiliwa kwa Besigye kumezusha hisia tofauti, huku wafuasi wake, Wanaharakati na makundi ya kiraia wakionya kwamba anahitaji huduma ya matibabu na wakitaka atolewe Gerezani. 

Wameongeza kuwa madhara yoyote yanayoweza kumpata akiwa kizuizini yanaweza kusababisha machafuko mabaya nchini humo ikizingatiwa kuwa hivi karibuni alianza mgomo wa kula.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *