Klabu ya Azam FC imepata tena, baada ya kuumia kwa golikipa wake mwingine Ali Ahamada, ambaye usiku wa kuamkia leo amepelekwa nchini Afrika Kusini kufanyiwa uchunguzi wa goti lake la mguu wa kushoto.

Mlinda lango huyo raia wa Ufaransa mwenye asili ya Comoro, alipata majeraha hayo wakati wa mechi ya Azam FC dhidi ya KMC, iliyomalizika Kwa Azam FC kushinda 5-0.
Licha ya Ahamada kupata nafuu na kumudu kucheza mchezo uliofuata wa Azam FC dhidi ya JKT Tanzania SC, lakini maumivu hayo yalizidi na sasa anaenda kufanyiwa uchunguzi wa kina nchini humo.
Huyo anakuwa kipa wa wa pili wa Azam FC kupata majeraha, baada ya jana Alhamis kipa wao mwingine Abdulai Iddrisu kuelekea pia nchini humo kwa uchunguzi zaidi wa bega lake la mkono wa kushoto.
Azam itaongozwa na makipa wawili ambao ni Zuberi Foba aliyecheza mara ya mwisho mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga na kuruhusu mabao mawili kwenye kipigo cha 2-0 na Yassin Hamiss aliyepandishwa kutoka timu ya vijana baada ya Wilbol Maseke kwenda KMC hadi pale watakapo rejea Ali na Idrisu.