Magari yapewa Ruksa kuanza safari saa 9 Usiku

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhrini (LATRA) imerudisha ratiba za ruti za saa 9 usiku kwa mabasi tisa ya kampuni ya Ally’s Star na Katarama Luxury. Awali Juni 19 mwaka huu LATRA walifungia mabasi ya kampuni hizo ratiba zinazoanza safari zake majira hayo kutokana na ukiukwaji wa sheria. Ilidaiwa kutokana na kifungu cha 5 (1) (b) na 6(b) cha sheria mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini sura ya 413 latra ina mamlaka na ina jukumu la kuuhisha na kufuta vibali na leseni za usafirishaji kwa kukuza usalama wa sekta zinazodhibitiwa kwa watumiaji wa huduma.

Akiongea na vyombo vya habari, Kaimu Mkuu wa kitengo cha mahusiano Salum Pazi alisema wamekuwa wakifatilia utoaji wa huduma wa mabasi hayo kwa ukaribu ikiwa na uzingatiaji ratiba zao za kuanza safari, utumiaji wa taarifa katika mfumo wa kufuatilia mwenendo wa magari, mwendokasi wa magari na matumizi ya kutufe cha uchambuzi wa dereva (I-Button). Mbali na hilo LATRA pia imetoa onyo kali kwa kampuni saba za mabasi ya abiri kutokana na ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu ikiwemo na mwendokasi uliopitiliza wakiwa safarini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *