Watu 12 wamefariki na zaidi ya 50 hawajulikani waliko baada ya mvua kubwa kusababisha korongo kuporomoka kwenye mto kusini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Maporomoko hayo ya ardhi yalitokea Jumamosi saa sita mchana katika eneo la Dibaya Lubwe katika mkoa wa Kwilu yalilisababisha udongo na vifusi kuanguka kwenye kingo za Mto Kasai na pia kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Mratibu wa asasi ya kiraia wa eneo hilo Arsene Kasiama amebainisha kwamba yaliwakumba watu waliokuwa wakiendelea na shughuli za biashara sokoni.
Gavana wa mpito Felicien Kiway amesema miili 12 imeondolewa kwenye vifusi mpaka sasa, wakiwemo wanawake tisa, wanaume watatu na kueleza kwamba matumaini ya kuwapata manusura ni madogo sana kwa sababu tukio hilo lilitokea saa 12 kabla na bado wanaendelea shughuli ya utafutaji kwenye udongo