Mafuriko yaliyopasua bwawa  yaua watu 42 Kenya

Watu 42 wamefariki katika mafuriko katika eneo la Mai Mahiu katikati mwa Kenya baada ya bwawa kupasuka hii leo na kwa mujibu wa maelezo ya polisi ni kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

Picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya X na vyombo vya habari vya Kenya, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya na mamlaka ya barabara kuu zimeonyesha matukio ya baada ya mafuriko, miti iliyokatika na gari moja lililokwama kwenye magogo na matope.

Kamanda wa polisi wa Naivasha Stephen Kirui Kufikia wakati huo(alipokuwa akiongea) walifanikiwa kupata miili 42, ikiwemo miili ya watoto 17, kufuatia tukio la asubuhi ya leo ambapo kingo za bwawa zililipasuka katika  eneo la Kijabe na shughuli za uokoaji na utafutaji zinaendelea.

Mapema Jumatatu ya leo Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema liliwapeleka watu kadhaa kwenye kituo cha afya Mai Mahiu kutokana na mafuriko hayo na hadi sasa idadi ya vifo kutokana na mvua kubwa na mafuriko tangu mwezi uliopita imefikia zaidi ya 140 nchini Kenya.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *